BARAZA LA MANISPAA ZANZIBAR LINAKUSUDIA KUWEKA KANUNI ZA KUIMARISHA USAFI

Baraza la Manispaa Zanzibar linakusudia kuweka kanuni za kuimarisha usafi na kuzisimamia kwa wakaazi wa mji ili kuuweka katika hali ya usafi na kuwa na mandhari nzuri ya kuvutia kwa wenyeji na wageni.

akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi wa baraza hilo Aboud Hassan Serenge amesema katika hatua za awali wameanza kuwahimiza wakaazi wa kikwajuni kusafisha mazingira wanayoishi na kusimamia wengine wasichafue hadi hapo kanuni zitakapotungwa na kuanza kufanyiwa kazi.

hatua hiyo imekuja kutokana na baraza hilo kutarajia kupokea ugeni kutoka mji wa Postdum Ujerumani ambao watatiliana saini mkataba katika mradi wa kuimarisha urafiki wa kidugu baada ya kumalizika kwa mradi wa mwanzo wa kuimarisha uhifadhi wa mazingira ambao ulihusika na kutengeneza bustani za mji na kujenga vibaraza vya kupumzika pamoja na Taa za Solar.

mradi huo wa kuimarisha udugu utahusu matengenezo ya Majengo ya Mjerumani yaliyopo Kikwajuni, Bustani ya Breeze Migombani, kitengo cha afya kwa maradhi ya Saratani, kutoa elimu kuhusu tatizo la maradhi hayo na kudumisha usafi katika Mji.