BARAZA LA MAULAMAA ZANZIBAR LIMEINGILIA KATI UGOMVI WA WAKAAZI WA KIJIJI CHA UKONGORONI

Baraza la Maulamaa Zanzibar limeingilia kati ugomvi wa wakaazi wa kijiji cha  ukongoroni uliohusishwa na imamni za kishirikina baada ya vijana kuzama baharini na wengine kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

wakizungumza katika Dua ya kurejesha imani kwa wakaazi wa kijiji hicho baraza hilo limesema jamii haipaswi kuyatumia mambo ya uchawi kwa vile yanazusha mfarakano inayohatarisha amani katika jamii.

wajumbe wa baraza hilo wakiongozwa na Naibu Mufti wa Zanzibar   Mahmoud mussa wadi amesema ni vyeme watu hao wakasafiana nia na kutafuta ufumbuzi wa tukio hilo bila ya  kuhusisha imani hizo kwavile hazikubaliki kiimani na hata kisheria.

katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa kusini unguja Dkt Idrissa Muslim Hijja amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo imeshitushwa na vitendo hivyo vya wakaazi wa kijiji hicho kushtumiana sababu za kishirikina kulikosababisha baadhi ya watu kukihama kijiji hicho.

amewataka vijana kuondoa hofu na kusiriki katika shughuli zao za kiuchumi kwa vile dua iliyosomwa imeweka kinga kwa pande zote.