BARAZA LA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO LA ZANZIBAR KUTASAIDIA KUPUNGUZA MATATIZO YA WAKULIMA

 

Waziri wa kilimo, maliasili mifugo na uvuvi mh Hamad Rashid Mohamed amesema kuundwa kwa baraza la taasisi ya utafiti wa kilimo la zanzibar kutasaidia kupunguza matatizo ya wakulima na itakuwa ni hatua nzuri ya kuingia katika uchumi wa viwanda.

Akizungumza na wajumbe wa bodi katika hafla ya uzinduzi wa baraza la hilo mh. Hamad amesema  lengo la kuundwa baraza la utafiti ni kusimamia na kutoa miongozo kwa  taasisi hiyo ya utafiti kutokana na zanzibar kuwa na  ardhi  nzuri ya kilimo  yenye  rutba na  hali ya hewa  inayostawisha  mazao mbali mbali.

Mwenyekiti wa baraza la taasisi hiyo ya utafiti  dr mwatima  abdalla juma  amesema kuundwa  kwa bodi  hiyo kutaweza kutatua masuala mengi katika sekta ya kilimo hivyo amemuomba waziri kushirikiana na wahusika ili taasisi hiyo iweze kuendelea kwa manufaa ya taifa.

Wajumbe wa baraza hilo wamesema hiyo ni hatua nzuri itakayosaidia kufanyika tafiti nyingi na kuondoa matatizo yanayozikabili sekta za kilimo, ufugaji na masuala ya baharini.