BARAZA LA TIBA ASILI ZNZ LINATOA TAHADHARI JUU YA DAWA ZISIZO THIBITISHWA

baraza la tiba asli zanzibar limewatahadharisha wananchi kutokubali kutumia dawa zilizokuwa hazijathibitishwa kwa mujibu wa sheria kwani ni hatari kwa afya zao.

mrajis wa baraza hilo Haji Juma kundi amesema  hivi sasa kumeibuka tena watu wanaouza dawa hizo katika mikusanyiko ya watu hasa misikitini wakati   zinahitaji kuwekwa katika sehemu maalum.

ametoa taarifa hiyo baada ya baraza hilo kukamata dawa mbalimbali zilizokuwa zinauzwa kiholela     zinazodaiwa kutengenezwa kienyeji na zinatishia maisha na tiba za wagonjwa.

mrajis kundi  amewataka wananchi kuachana na dhana kuwa dawa hizo ni za sunna wakati ni za miti shamba  zinazohitaji utaratibu maalum wa kutumiwa huku akiahidi  baraza hilo  litaanza kuchukuwa hatua kali kwa wanaokaidi.

baadhi ya watu waliokamatwa wakiuuza dawa hizo wamekiri kuuza dawa hizo kinyume cha sheria huku wakiomba  wenzao kuwa wakweli.