BARAZA LA VIJANA TAIFA KUWA NA UMOJA, USHIRIKIANO NA UPENDO

 

Waziri wa vijana sanaa utamaduni na michezo zanzibar balozi ali karume amewataka baraza la vijana taifa kuwa na umoja, ushirikiano na upendo kwa lengo la kuleta maendeleo nchini yakiwemo ya utamaduni, sanaa na michezo.

Akizungumza na baraza hilo afisini kwake migombani, balozi karume amesema jukumu kubwa la kijana yoyote ni kuchangia maendeleo ya taifa lake yakiwemo na mambo ya michezo na utamaduni huku akiwasisitiza kuendelea kusoma na kujifunza.

Balozi karume amewasisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano huku akiwapa salamu zao kutoka kwa mh rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohammed kwa kuwa anawajali ndio mana kaunda wizara hiyo maalum ambayo itasaidia vijana pamoja na sanaa, utamaduni na michezo.

Nae katibu mkuu wa wizara ya vijana utamaduni sanaa na michezo omar hassan king amezungumzia ujio wa baraza hilo wizarani kwao huku akisema wanatarajia kukutana na wadau wote wa sanaa utamaduni na vyama vya michezo.