BARAZA LA VIJANA WA TUMBATU VIMESHIRIKI MAZOWEZI YA PAMOJA

 

 

Vikundi  vya  mazoezi  na baraza  la  vijana  wa  tumbatu  vimeshiriki mazowezi ya pamoja na kuzinduliwa rasmi na  mwakilishi  wa  jimbo  hilo  haji omar  kheri.

Wakizungumza katika uzinduzi huo vikundi hivyo vimesema  vinakabiliwa na ukosefu wa mipango ya kuanzisha mashindano yatakayoibua vipaji na kushiriki mashindano nje ya tumbatu ambayo yatajenga ushirikiano zaidi.

Akizindua  vikundi hivyo mwakilishi haji omar  kheriamesma tayari mpango  wa  kuanzisha  ligi  ya  jimbo  kwa  lengo  la  kuimarisha   umoja  na  kuibua  vipaji  vya  michezo umeshaandaliwa na karibuni utaanza.

Ameahid  kuvitafutia  ufumbuzi  kero za vikundi  hivyo ili  kuimarisha  zaidi  michezo  tumbatu vijiji jirani.