BARAZA LA WATUMIAJI WA HUDUMA YA MAJI NA NISHATI LIMEZINDULIWA

 

Waziri wa nishati   maji na ardhi mhe salama aboud talib amelizindua barazala mwanzo la watumiaji wa huduma ya maji na nishati.

Pamoja na mambo mengine baraza hilo litakuwa n a kazi ya  kuwasaidia wananchi  katika utoaji wa  malalamiko yao na ili yafanyiwe kazi.

Akilizindua baraza hilo katika afisi za zura ziliopo maisra   mhe, salama amesema  uwepo wa baraza hilo utaleta ufanisi wa utendaji kazi na tija  kwa serikali na a kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu  katika upatikanaji wa huduma hizo muhimu kwa jamii.

Mhe salama amefahamisha kuwa licha ya uwepo wa malalamiko kwa kufanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa  wa upatikanaji wa huduma za maji na umeme  serikali  imekuwa ikijitahidi kuondosha kadhia hizo  ili kuona wananchi wake hawapati shida .

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa maji nishati na gesi  haji kali haji  akaelezea namna zura inavyosimamia majukumu yake ya kazi na kuahidi baraza hilo kufanya kazi zake vizuri .

Wajumbe wa baraza hilo akizungumza kwa niaba ya wenzake i ndg mahamoud mohd amemuhakikisshia mhe waziri kuwa watasimamia vyyema majukumu ya bazraza hilo. Zinawanufaisha wananchi  wote