BARAZA LA WAWAKILISHI KUJADILI BAJETI YA SMZ 2017/2018

 

Mkutano wa sita wa baraza la wawakilishi unatarajiwa kuanza jumatano ijayo ambapo pamoja na mambo mengine utajadili bajeti ya serikali ya mwaka 2017 /18.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katibu wa baraza hilo raya issa mselem amesema maswali 182 pia yataulizwa na kujibiwa na kuwasilishwa miswada mitano ikiwemo miwili ya dharura.

Ameitaja miswaada hiyo ni wa sheria ya marekebisho ya sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 2015, mswaada wa kufuta sheria ya ushuru wa stemp na kuweka sheria mpya na mswaada wa sheria ya ushuru wa bidhaa.

Shughuli nyengine itakayofanyika katika kikao hicho ni kuwasilishwa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali.