BARAZA LA WAWAKILISHI LINATARAJIWA KUANZA KIKAO CHAKE CHA KAWAIDA JUMATANO WIKI HII

Baraza la wawakilishi zanzibar linatarajiwa kuanza kikao chake cha kawaida jumatano wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine kitajadili na kupitisha miswada ya sheria.
Katibu wa baraza hilo raya issa mselem akizungumza na waandishi wa habari afisini kwake chukwani amesema masuala 113 ya wajumbe wa yataulizwa na kujibiwa.
Aidha amesema miswaada ya isheria minne itasomwa kwa mara ya pili na baadae kujadiliwa na wajumbe katika mkutano huo wa baraza la tisa .
Raya ameitaja miswada hiyo kuwa ni pamoja na mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya wakala wa usafiri na matukio ya kijamii,mswada wa kuanzisha wakala wa maendeleo ya viwanda vidogo vidogo,mswada wa marekebisho hya sheria mbali mbali na mswada wa sheria ya kufuta sheria ya uchaguzi ya mwaka 2017