BEI YA KAMBA YA USUMBA BADO IKO CHINI KATIKA UUZWAJI

 

 

hali ya bei ya kamba ya usumba bado iko chini katika uuzwaji ukilinganisha na ugumu wa kazi hiyo.

kamba ni bidhaa inayotokana na mali ghafi ya makumbi, ambayo huzikwa chini ya bahari kwa kipindi kisichopungua miezi sita hadi mwaka mmoja hadi kupatikana kamba yenyewe.

ugumu wa kazi hiyo hakiendani na kipato halisi, kwani humlazimu mtengenezaji kutumia gharama na  muda mwingi kukaa baharini.

zbc ambayo imewashuhudia akinamama wa kizimkazi dimbani ambao ndio aghlabu wanajishughulisha na biashara hiyo wakielezea hatua zinazopitia kupatika kamba ambayo hutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kufungia kuni na matumizi mengine.

wamesema wanashindwa kuzalisha kwa wingi bidhaa hiyo kutokana na kutokuwa na soko la uhakika pamoja na bei ndogo wanayouza kwani futi 20 huuzwa kwa shilingi elfu 2000 ikilinganishwa na masafa wanayotembea kutafuta mali ghafi ya makumbi.

hivyo wameiomba serikali kuwasaidia kupata soko la uhakika la kuuza bidhaa yao hiyo pamoja na kuwapatia mashine ya utengenezaji ili kujinusuru na hali za kiafya.

akizungumzia suala hilo sheha wa shehia ya kizimkazi kassim…..amesema serikali ya shehia imewasadia kinamama hao eneo la kufanyia shughuli zao ingawa eneo hilo halitoshelezi.