BEIT EL AJAIB LAANZA KUFANYIWA MATENGENEZO

 

 

Idara ya makumbusho na mambo ya kale imeanza  zoezi la ufunguaji wa nguzo zilizozunguka  jengo la  kihistoria  la beit el ajaib   kwa  lengo la kutaka kulifanyia matengenezo  hapo baadae.

Msimamizi   wa jengo hilo  ambae ni mfanyakazi   wa nyumba za   makumbusho    ali dishon   ameiambia zbc kuwa  ufunguaji wa nguzo hizo  unaofanywa na kampuni ya zico limited unatarajiwa kuchukuwa muda wa mwezi mmoja.

amesema   wameanza kufungua  nguzo za jengo  hilo katika hatua ya awali  badala kubomoa ili kuliokoa  kuzidi  kuporomoka  sehemu nyengine ambapo ujenzi wake utaanza baada ya kumaliza hatua hiyo

Hata hivyo amesema  katika ujenzi huo wataalamu watalazimika kufanyia utafiti udongo uliotumika katika kuta za  nyumba hiyo kabla ya kuanza  matengenezo yake.