BIMA KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA KAMPUNI ITAKAYOSHINDWA KUMLIPA MTEJA

 

Mamlaka ya bima zanzibar  imesema haitosita kumchukulia hatua za kisheria kampuni yoyote ya bima itakayoshindwa kumlipa mteja wake wakati anapopata majanga mbali mbali.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mamlaka hiyo, mara baada ya kikao na wadau wa bima katika kilele cha kuelekea siku ya maadhimisho meneja wa mamlaka hiyo nd.muhamed khamis, amesema hakuna sababu ya kampuni hizo kukaidi makubaliano ya mteja ambaye amekuwa akifuata masharti.

Akizungumzia kuhusu udanganyifu wa kuwepo kwa bima feki za vyombo,nd. Muhamed amesema mamlaka ya bima imeweka utaratibu maalum wa utumiaji kwa njia ya mitandao ili mwananchi kuweza kubaini bima isio halali.

Katika kikao hicho wadau wa bima, ikiwemo shirika la bima zanzibar,mayfair,jubilee,nic,britam,aar,sanlam na uap zilizopo zanzibar wamesema wamekuwa wakitekeleza majuku yao ipasavyo na kuwataka wananchi kujisajili ili kuweza bima hizo kuwasaidia katika maisha yao.

Maadhimisho ya siku ya bima zanzibar huazimishwa ifikapo juni 23 katika viwanja vya mnara wa kumbukumbu kisonge.