BINGWA AMEJULIKANA AMBAYE NI CHELESA VITA YA KUWANIA NAFASI YA NNE

 

Wakati ligi kuu soka nchini uingereza ikielekea ukingoni na bingwa tayari amejulikana ambaye ni chelesa  vita ya kuwania nafasi ya nne inaonekana kujitokeza  kwa timu za Liverpool,Arsenal na Manchester city  kupigana vikumbo katika nafasi hizo kwa kupata nafasi ya kucheza mashindano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu ujao

Arsenal jana wakiwa ugenini wamefanikiwa kuichabanga Stoke city kwa magoli 4-1 na kufufua matumaini yao kuingia top 4

Huku Manchester city nayo ikiwatandika  Leicester city kwa 2-1 nao kufanikiwa kujichimbia  kwenye  nafasi ya 3

Kwa upande wao Majogoo wa jiji Liverpool wakichomoza na ushindi dhidi ya  westham wa mabao 4-0

Wakati nayo timu ya hull city leo imeungana na timu za sunderland na midlesbrough kushuka daraja hadi ligi daraja ka kwanza kwa msimu ujao kufuatia kupoteza  mchezo dhidi ya christal palace kwa magoli 4-0

Chelsea chini Antonio Conte imeweka rekodi ya kuwa klabu ya pili kutwaa ubingwa wa EPL mara nyingi ambapo imetwaa mata tano nyuma ya Manchester United iliyotwaa mara 13.

Chelsea imeweka pia rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutwaa ubingwa wa EPL siku ya Ijumaa tangu Arsenal ilipofanya hivyo katika uwanja wa Anfield 1989 huku Antonio Conte akiwa meneja wa nne kutoka Italia kushinda taji hilo baada ya Ancelotti, Roberto Mancini na Claudio Ranieri.