BODI MBALIMBALI KUSHIRIKIANA WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

Waziri wa habari, utalii,utamaduni na michezo MH Rashid Ali Juma amezitaka bodi mbalimbali za wizara hiyo kushirikiana kwa karibu wanapotekeleza majukumu yao ili kuongeza ufanisi.
Akizungumza wa wenyeviti wa bodi hizo katika kikao cha dharura mh rashid amesema ushirikiano huo pia uhusishe ziara ziara kati ya ofisi zao ili kuleta mabadiliko ya kiutendaji.
Aidha muheshimiwa huyo amezikaribisha bodi hizo kuwa ofisi yake ikotayari kupokea ushauri wa kikazi muda wote kwa lengo la kufanikisha maendeleo ya wizara.
Wakichangia katika kikao hicho wenyeviti mbalimbali wabodi wakiwemo mwenyekiti wa bodi ya utangazaji na wengine wamesema wamefurahishwa na kikao hicho kwani kitaleta mabadiliko makubwa pamoja na kumshauri waziri kwamba awe na tabia ya kukutana kila baada ya muda kuendeleza kikao hicho.