BODI MPYA YA KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA KUZITAFUTA NA KUZISIMAMIA MALI ZOTE ZA KAMISHENI

 

 

Waziri wa nchi ofisi ya rais katiba, sheria, utumishi wa umma na utawala bora mh. Haroun ali suleiman ameitaka bodi mpya ya kamisheni ya wakfu na mali ya amana kuzitafuta na kuzisimamia mali zote za kamisheni hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa bodi mpya ya kamisheni ya wakfu na mali ya amana, waziri haroun ametaka bodi hiyo kuwa na kumbukumbu sahihi za mali za kamisheni, kujua zilipo na wanaozisimamia na kama zipo katika mikono salama.

Ameishauri bodi hiyo mpya chini ya mwenyekiti wake professa hemed rashid hikmani kuandaa utaratibu wa kutafuta fedha za kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo.

Aidhaa amezitaka taasisi zinazoandaa safari za hijjah, kuandaa mazingira mazuri ya safari hizo ili kuwaondoshea usumbufu mahujaji wakati wa safari na wanapotekeleza ibada hiyo nchini saudi arabia.

Mwenyekiti wa bodi ya kamisheni ya wakfu na mali ya amana aliemaliza muda wake dkt. Issa haji zidi amesema bodi yake ilifanyawajibu wa kuimarisha kamisheni licha ya changamoto walizokutana nazo.

Ameishauri wizara ya katiba, sheria, utumisha wa umma na utawala bora kukasimu baadhi ya kazi za kamisheni ya wakafu na mali ya mani katika ngazi za wilaya.

Ae mwenyekiti mpya wa bodi hiyo prof. Hemed rashid hikmani ambae alikuwa makamu mwenyekiti wa bodi iliyopita ameahidi kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa ili kuhakikisha kamisheni inatekeleza majukumu yake ya msingi waliyokabidhiwa na serikali