BODI YA BANDARI IMEFANIKIWA KIASI KIKUBWA KUTATUA MATATIZO MENGI

 

Mwenyekiti wa bodi ya shirika la bandari zanzibar ndugu salmin senga salmin  amesema bodi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa     kutatua matatizo mengi yaliyokuwa yakilikabili shirika la bandari katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Akizungumza na wafanyaazi wa shirika hilo katika hafla ya kuwatabulisha wajumbe wapya wa shirika hilo ndugu senga amesema

Bodi mpya itaendelea kumaliza changamoto zilizobaki ili kwa faida ya shirika ,wafanyakazi na serikali kwa jumla.

Amewaomba wafanyakazi wa shirika hilo tegemeo la kuinua uchumi wa zanzibar kuipa ushirikiano bodi hiyo ili lengo kupatikana ufanisi liweze kupatikana.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la bandari zanzibar cpt juma abdalla juma amesema bodi iliyomaliza muda wake ilifanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kutembelea minara ya kuongozea vyombo vya baharini  na shughuli nyingine za shirika.

Afisa usalama wa shirika la bandari masoud haji omar amelishauri shirika kuwasaidia matibabu wafanyakazi wanapopata maradhi  sambamba na kuwaongezea kiwango cha posho la likizo kwani wanacholipwa hivi sasa ni kidogo hasa ukizingatia wafanyakazi wengine  kwao ni tanzania  bara