BODI YA UKAGUZI INASIKITISHWA NA UFANYAJI KAZI WA HOSPTALI BINAFSI KWA KUJALI MBELE MASLAHI YAO
katika hatua nyengine ya ukaguzi wa hosptali binafsi unaoendelea kufanya na bodi ya ukaguzi imesema inasikitishwa na ufanyaji kazi wa hosptali hizo binafsi kwa kujali mbele maslahi yao pasi kutii masharti wanayopewa na bodi hiyo wakati wanapoomba ridhiaa ya kufungua vituo hivyo .zoezi hilo la ukaguzi liloanzia jumbi wakati daktari dhamana wa kituo hicho ametakiwa kukifunga kituo hicho kwa kutokuwa na leseni ya udaktari pamoja na kutokuhifadhi vizuri mazingira ya taka sambamba na kituop cha afya zuha kiliopo fuoni nacho kimetakiwa kusitisha huduma za kiafya kwa makosa mbalimbali likiwemom la muuguzi kutoa tiba za maabara na sehemu ya dawa wakati ni nesi .
akizungumzia makosa hayo mratibu wa bodi ya ukaguzi dr faiza kassim amekuwa na haya ya kusema kuhusiana na hyali hiyo. nao wananchi waliofata huduma katika kituo cha afya jumbi wakawataka wamiliki kufuata masharti yaliowekwa na bodi ili kuondosha usumbufu kwa wagonjwa wanaofika pale wa matibabu .zoezi hilo likaendelea na kukaguzi katika vituo vyengine mbalimbali na ndipo wakabaini kituo cha afya cha jozia dispensary kiliopo fuoni meli tano kinaendesha huduma wakati bado maombi yake kwa bodi hayajajibiwa ya kupatiwa leseni na kutakiwa kukifunga mara moja kwani kimevunja sheria zilizowekwa na bodi hiyo kama anavyoeleza msaidizi mrajisi wa ukaguzi wa bodi ya hosptali binafsi ndugun khamis makame jumla ya vituo sita vimekaguliwa na kufungwa vitatu kati ya hivyo na vilivyosalia kufungwa bodi imeridhika navyo na utoaji wa huduma kwa wananchi