BOSCO NTAGANDA AMETOA USHAHIDI KATIKA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA ICC.

 

Aliyekua kiongozi wa waasi nchini congo bosco ntaganda ametoa ushahidi katika mahakama ya kimataifa ya icc.

Ntaganda  amesimaia kizimbani ikiwa ni kiasi miaka miwili tangu kuanza keshi hiyo  anashutumiwa kutekeleza uhalifu dhidi ya binaadam unaodaiwa kutekelezwa na vikosi vyake.

Mashtaka yanasema kuwa kati ya mwaka 2002 na 2003 vikosi vyake vya uasi walitekeleza mauaji katika eneo la ituri na kuwabaka raia ambapo pia mwaka 2015 alikutwa na hatia kwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwasajili watoto wa umri wa chini ya miaka 15 kwenye jeshi na makosa mengine.

Kesi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa miezi kadhaa na iwapo ntaganda atakutwa na hatia atahukumiwa kifungo cha mpaka miaka 30 gerezani.