BUNGE LA UINGEREZA LAIDHINISHA MUSWADA WA KUJITOA UMOJA WA ULAYA

 

Bunge la Uingereza limetoa idhini ya mwisho ya sheria muhimu katika hatua ya mchakato wa kuelekea kutaka kujitoa katika jumuiya ya Ulaya.

Serikali ya Uingereza inapanga kuanza hatua rasmi za kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Hatua hii inatarajiwa kuwa na utata kufuatia tangazo la Scotland linalodai kuwa wanampango pia wa kuwa na kura ya maoni kuhusiana na kujitenga kwao na Uingereza na kisha kuwa taifa huru.

Chama upinzani cha Liberal kimesema serikali imeshindwa kuonyesha msimamo juu ya haki za raia wa EU wanaoishi nchini Uingereza na kutoa wito kwa makundi mbali mbali kusisitiza juu ya mabadiliko.