CARLES PIGMONT AMEONEKANA HADHARANI KWA MARA YA KWANZA

 

Aliyekuwa kiongozi wa serikali iliyoondolewa madarakani ya jimbo la catalonia carles pigmont ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza nchini ubeligiji tangu alipoonekana mahakamani kufuatia amri ya kukamatwa kwake iliyotolewa na serikali ya uhispania.

Pigmont ameungana na wanasiasa wengine 200 wa catalonia katika eneo moja la makumbusho ya sanaa mjini brussels.

Pigmont amesema katika mahojiano kuwa amepanga kuongoza muungano wa makundi ya kisiasa katika harakati za kudai uhuru wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mwezi desemba na ametoa wito kwa waziri mkuu wa uhispania mariano rajoy kusitisha kutumia ibara ya 155 ya katiba inayoipa mamlaka serikali kuu ya uhispania kulitawala jimbo hilo moja kwa moja.

Kwa upande mwingine msemaji wa kansela wa ujerumani angela merkel, ameungana na viongozi wengine wa ulaya na marekani akisema hatambui hatua ya jimbo la catalonia kujitangazia uhuru wake.