Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

KUDHIBITI VITUO AU WATU WANAOFUNDISHA LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI

Mkuu wa idara ya kiswahili kwa wageni chuo kikuu cha taifa zanzibar dkt. Zainab ali iddi ameiomba serikali kuwasaidia kudhibiti vituo au watu wanaofundisha lugha ya kiswahili kwa wageni bila ya kibali maalum kutoka  serikalini ili kudhibiti matumizi mabaya ya lugha ya kiswahili.

Dk zainab amesema hayo wakati akizungumza na zbc baada ya kusikiliza tafiti zilizowasilishwa  zilizowasilishwa na wanafunzi hao kutoka beijing nchini china wakiwa katika za mwisho za kumaliza masomo yao ya miezi minne ya kujifunza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu cha taifa cha zanzibar.

Wanafunzi wanaojifunza lugha ya kiswahili katika chuo kikuu cha taifa zanzibar  kutoka beijing china wamesema zanzibar ni sehemu nzuri ya kujifunza lugha ya kiswahili kwani katika kipindi cha mienzi minne wamejifunza misamiati mingi ukilinganisha na miaka miwili waliyojifunza kiswahili wakiwa china.

Pia wanafunzi hao watano waliwasilisha tafiti zao walizozifanya kuhusu uchoraji wa tingatinga, mchango wa siti bint saad katika maendeleo ya taarab zanzibar ,utalii ni uti wa mgongo katika maendeleo ya taifa, na mlingano na tofauti baina ya majengo ya china na majengo ya zanzibar.

 

JUMUIYA YA MAGARI MAWE NA MCHANGA KUPELEKEWA HUDUMA MUHIMU KATIKA ENEO JIPYA

Jumuiya  ya magari mawe na mchanga wameiomba serikali kuwapelekea huduma muhimu katika eneo jipya walilohamishiwa huko jumbi ikiwa ni pamoja na kuwekewa kifusi ili waweze kufanya shughuli zao katika mazingira bora.

Kionozi wa Jumiya hiyo ndugu Hassan Ramadhan Kassu ameasema wamefarijika na hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Mkoa  Mjini Magharibi ya kuwapatia eneo hilo badala ya Mwanakwerekwe, hata hivyo wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa huduma ya choo, maji na sehemu ya kuuza biashara  kwa kinamama.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mawe na mchanga wamesema hali ya biashara sio mbaya na wametoa wito kwa  wananchi  kufatia mahitaji yao katika eneo hilo na hakuna ongezeko lolote la bei.

Aidha wameiomba serikali kuruhusu tena uchimbaji wa mchanga, wamesema tangu kuzuiwa kwa uchimbaji wa mchanga biashara ya mawe imepungua pamoja na kuathiri ajira  za vijana wengi .

Wakati  huo huo wameiomba serikali kuzuia uchimbaji  wa mchanga kwa kutumia skaveta pale mchanga utakaporuhusiwa tena kuchimbwa kwani uchumbaji wake unaharibu sana  mazingira na kushauri kutumia uchimbaji wa zamani wa kutumia pauro.

Akielezea kuhusu changamoto zilizotajwa na wafanyabiashara ya mawe na mchanga Mkurugenzi Baraza la Magharibi B  Ndugu Ali Abdalla  Natepe amesema wanatambua uwepo wa kasoro hizo na wameanza kuchukua hatua ya kuzipatia ufumbuzi wake .

Amewataka wafanyabiashara hao waendelee kushirikiana na Baraza la Manispaa juu kuliimarisha eneo hilo.

Amesema pia suala la usafi wa maeneo hasa pembezoni mwa barabara litaendelea tena hivi karibuni katika njia mbalimbali za Manispaa hiyo na kutoa wito kwa watu walioweka magari mabovu  na majiko ya umeme, mafriji na bidhaa nyengine zilizotumika kuziondoa bidhaa zao ili kutoa nafasi ya kutumika vizuri barabara hizo.

KISIWA CHA UZI KINAIMARIKA KWA KUPATA HUDUMA ZA MAENDELEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kupitia serekali anayoiongoza atahakikisha kuwa kisiwa cha uzi kinaimarika kwa kupata huduma za maendeleo ikiwemo kujenga barabara na daraja kutoka unguja ukuu kaepwani hadi uzi.

WALIMU WA SKULI KUTUMIA ZAIDI ZANA NA VIELELEZO KATIKA KUFUNDISHA WANAFUNZI

Katibu mkuu wizara elimu na mafunzo ya amali dk idrissa muslim hija amesema wakati umefika  kwa walimu wa skuli kutumia zaidi zana na vielelezo katika kufundisha wanafunzi badala ya kutumia chaki, mdomo na ubao pekee.

Dk muslim amesema hayo wakati akisoma  hotuba ya waziri wa elimu na mfunzo ya amali  katika chuo kikuu cha taifa zanzibar (suza) kampasi ya nkrumah kwenye ufunguzi wa maonesho ya zana za kufundishia na kujifunzia  .

Amesema iwapo vitendea kazi na vielelezo vitatumika vizuri na kwa muda sahihi kuna uwezekano mkubwa kiwango cha ufahamu kwa wanafunzi kuongezeka na kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya taifa na kuinua kiwango cha elimu.

Mkuu wa skuli ya elimu ya suza dk. Maryam jaffar ismail amesema wanafanya juhudi ya kuwaandaa walimu wanaosoma chuoni hapo kutengeneza zana za kusomeshea kwa kutumia vitu vilivyopo katika mazingira yaliyowazunguka ambavyo havina gharama kubwa ili kuwasaidia wanafunzi wao na kuongeza ufanisi katika kazi hiyo.

Amesema changamoto inayoikabili kada ya elimu nchini ni vijana wengi kukataa kujiunga na kada hiyo na wanaojiunga ni vijana wanaokosa  masomo katika fani nyengine jambo ambalo alisema sio sahihi.

Katika risala ya walimu wanafunzi wa kada ya ualimu suza walisema wanakabiliwa na tatizo la sehemu ya kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia na sehemu ya kuzihifadhi baada ya kuzitengeneza hivyo wamekiomba chuo kutafuta sehemu maalum  kwa kazi hiyo.

 

Powered by Live Score & Live Score App