Category Archives: Kitaifa

Habari za ndani ya nchi

TUMETAKIWA KUDUMISHA USAFI KATIKA SHEHIA ZETU ILI KUJIKINGA NA MADHARA MBALI MBALI

Mabaraza  ya vijana wilaya Magharibi “B” yametakiwa kudumisha usafi katika shehia zao ili kujikinga na  madhara mbali mbali yanayoweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na mstahiki meya manispaa Magharibi “B” ndugu maabadi ali maulid wakati alipokuwa akikabidhi vifaa vya usafi kwa baraza la vijana shehia ya mbweni wilaya yaMagharibi “B”’ amesema baraza la manispaa magharibi ‘b” linaungana na sera ya serikali ya kuwajali vijana ya kuwasaidia kupitia ngazi mbali mbali ikiwemo kwenye shughuli za usafi hivyo amewataka vijana hao kukitunza  vifaa walivyopatiwa ili lengo la kuweka mji safi liweze kufikiwa.

Afisa mipango manispaaMagharibi “B” ndugu saumu daniel yussuf amewaomba vijana kuvitunza na kuvitumia ipasavyo  vifaa hivyo  huku na kuahidi kshirikiana nao katika shuguli mbali mbali ili kuleta maendeleo katika maeneo ya manispaa hiyo

Akizungumza  baada ya makabidhiano  hayo ya vifaa hivyo mwenyekiti baraza la   vijana shehia ya mbweni  ndugu  othman haidar wameushukuru uongozi wa baraza la manispaa kwa msaada huo kwani vitaweza kuwasidia katika shughuli zao katika shehia yao

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na  mabero, mapauro, viatu na vifaa vyenginevyo kwa lengo la kusaidia mabaraza katika shehia mbali  mbali hasa katika shughuli za usafi.

WATUMISHI WA TAASISI ZA UMMA NCHINI KUWA TAYARI KATIKA KUYARIPOTI MATENDO YOTE MAOVU

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka  Wananchi pamoja  na watumishi wa taasisi za umma nchini kuwa tayari katika kuyaripoti matendo yote maovu yanayoonekana kwenda kinyume na Maadili ya Taifa.

Amesema wapo baadhi ya Watu wachache wamekuwa wakirejesha nyuma jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya Rushwa, jambo ambalo linapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria  na kanuni za Nchi

Akizungumza na Wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binaadamu katika Kiwanja cha Michezo Gombani Chake Chake Pemba Balozi Seif amesema tatizo la Rushwa katika Jamii na mgongano wa Kimaslahi yanaendelea kuathiri Nchi nyingi Duniani ikiwemo Tanzania.

Balozi Seif alisema  vitendo hivyo hudhoofisha upatikanaji wa Haki za Binaadamu kwa kiwango kikubwa na kurejesha nyuma jitihada za kuimarisha misingi ya Haki na Utawala Bora.

Balozi Seif amesema kupitia   ripoti iliyotolewa Mwaka  2017 inayoangazia mapambano dhidi ya Rushwa inaonyesha Tanzania kuwa ni Nchi ya Pili ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na jirani yake Rwanda katika mapambano dhidi ya Rushwa.

Huku kwa upande wa  Kimataifa Tanzania inashikilia nafasi  ya 103 kutoka nafasi ya 116  dhidi  ya vitendo hivyo ambapo aliwanasihi  Wananchi kushirikiana  na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa  ili kujiwekea nafasi ya kufanya vizuri katika ripoti itakayotolewa .

Pia  balozi seif  aliwanasihi wasimamizi wa Tenda kuwa makini katika kusimamia haki na Uadilifu kwa wanaoomba sambamba na kuepuka kuitia hasara Serikali .

Akisoma Risala Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nd. Assaa Rashid amesema misingi ya Utawala Bora itaimarika zaidi iwapo Jamii itajikita katika kuziba Mianya ya Rushwa na kuongeza Uwajibikaji.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye kilele cha Maadhimisho hayo ya Siku ya Maadili na Haki za Bianaadamu Waziri wa Nchi Ofisi yua Rais, Katiba, Sheria ,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Haroun Ali Suleiman aliwaomba Watendaji wanaosiamamia Suala la Maadili kuwa na Lugha nzuri katika kuuhudumia Umma.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyapokea Maandamano ya Taasisi mbali mbali zinazosimamia Maadili na Haki za binaadamu  pamoja na Wananchi katika kuadhimisha sherehe hizo.

Ujumbe wa Mwaka huu wa Siku ya Maadili na Haki za Binadamu unasema “ Tuimarishe Uadilifu, Uwajibikaji, Haki za Binadamu na Mapambano dhidi ya Rushwa kwa Maendeleo ya Taifa.

 

BARAZA LA MJI CHAKE KUFUATILIA KIWANGO CHA FEDHA KINACHOTOLEWA KATIKA KWARE

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Mh. Shamata Shaame Khamis ameliagiza baraza la mji chake chake kufuatilia kiwango cha fedha kinachotolewa katika kware ya Vitongoji ili kujua kuwa  kinakwenda na uhalisia na wananchi wanafaidika vipi katika eneo hayo.

Amesema serikali imeweka mashine za kukusanyia fedha kwa lengo la kudhibiti mapato yasipotee, kwani ndizo zinazotumika  katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi.

Mh. Shamata ametowa agizo hili baada ya kukagua kware ya uchimbaji wa kifusi Vitongoji na kupata maelezo kutoka kwa muwekezaji wa eneo hilo na uongozi wa wilaya na kusisitiza haja ya kuvitafuta vyanzo vipya ili kuongeza kiwango cha ukusanyaji.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Nd. Rashid Hadid Rashid amesema wataendelea kusimamia eneo la kwareni ili kuhakikisha baada ya kuchimbwa linafukiwa ili eneo liweze kutumika katika shughuli za uzalishaji.

Kwa upande wake Nd. Khamis ambae amekodi eneo hilo amelalamika ubovu wa barabara kuwa ni usumbufu kwa madereva wanaokwenda kufuata huduma hiyo.

MUONGOZO WA UKAGUZI WA USALAMA NA AFYA KAZINI NI JAMBO LA HESHIMA KATIKA SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA.

Mwenyekiti wa kamisheni ya utumishi wa umma Mhe.Balozi Mohammed Fakih amesema muongozo wa ukaguzi wa usalama na afya kazini ni jambo la heshima katika sekta ya utumishi wa umma.

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua  mafunzo ya kujenga uwelewa na kuutangaza muongozo ,wa ukaguzi wa usalama na afya kazini katika utumishi wa umma, yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali uliopo maisara wilaya ya mjini.

Balozi Fakih amesema muongozo huo utasaidia kuimarika kwa hali ya usalama na afya kazini na sekta ya umma kutekeleza majukumu yake kuzingatia viwango vya kazi vya kitaifa na sheria za kazi kufikia viwango vya kimataifa..

Akiwasilisha mada ya muongozo wa ukaguzi katika sehemu za kazi  mkurugenzi wa usalama na afya kazini mwalimu Suleiman Ali amesema usalama na afya kazini inajikita zaidi katika kinga ili kuepuka madhara katika sehemu za kazi.

Mapema katibu wa kamisheni ya utumishi wa umma ndugu Mdungi Makame Mdungi amesema umuhimu wa muongozo ni kuhakikisha watumishi wa umma wa umma wanafanya kazi katika mazingira yaliyo salama na kutoweza kuletea madhara ya kiafya.

Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha maafisa wa utumishi wa taasisi za serikali

Powered by Live Score & Live Score App