Category Archives: Michezo na Burudani

WATOTO WAHAMASISHWA KUSHIRIKI CHEMSHA BONGO ZA DINI YA KIISLAM

Wazazi na walezi wametakiwa kuwahamasisha watoto wao kushiriki kikamilifu katika kujibu masuali mbalimbali ya dini ya kiislamu kwa lengo la kuijua kwa undani dini yao.

Wito huo umetolewa na naibu katibu mkuu anaeshughulikia habari katika wizara ya habari utalii na mambo ya kale Shekhe Saleh Yussuf Mnemo katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa chemsha bongo ya ramadhani.

Shekhe Mnemo amesema kipindi cha chemsha bongo ya ramadhani ni chachu ya kuwakumbusha watoto na waislamu kwa ujumla kuifahamu na kuielewa vyema dini ya kiislam.

Nao wafadhili wa kipindi hicho wamewataka watayarishaji wa kipindi hicho kuandaa utaratibu wa kipindi hicho kuonyeshwa ZBC TV.

Akisoma risala ya watayarishaji wa vipindi vya ramadhani Zanzibar Bi Aziza Hassan amesema kipindi hicho kina changamoto nyingi ikiwemo kukosa wafadhili wa kutosha ili   kuwapatia zawadi washindi.

MICHEZO NI CHAKULA CHA MWILI NA HUWAEPUSHA VIJANA NA VITENDO VIOVU

Wazee wametakiwa kuwapa ruhusa vijana wao  wanapotaka kujifuza michezo kutokana na kuwa michezo ni chakula cha mwili na inawaepusha na vitendo viovu.

Ameyasoma hayo mwalimu wa mpira wa kikapu wa skuli ya urafiki na kijichi katika ufunguzi wa bonanza wa mpira huo uliyo fanyika katika skuli ya urafiki.

Rais wa tbf pamoja na mkurugenzi wa idara ya michezo na mafunzo ya amal wamesema mipango ya kuwaendeleza vijana itaweza kutowa wachezaji wa klitumikia taifa kwa baadae.

Mapema wanafunzi hao wakisoma risala wamesema changamoto kubwa zinazo wakumba ni pamoja na kutpewa ruhusa na kutokuwa na vifaa vya mchezo huo.

HATUA YA ROBO FAINALI LIGI YA VILABU BINGWA BARANI ULAYA

Hatua ya robo fainali ligi ya vilabu bingwa barani ulaya inatarajiwa kuanza kesho mzunguko wa kwanza kwa kuchezwa michezo miwili kwenye viwanja 2 tofauti majira ya saa 4:00 za usiku.

Majogoo wa anfield timu ya liverpool watakuwa na kazi kucheza na timu ya fc porto ya ureno mchezo utakaochezwa huko uengereza kwenye uwanja wa anfild.

Mchezo mwengine kesho muda huo huo utawakutanisha miamba miwili ya england kati ya totenhmah hotspurs dhidi ya manchester city.

Mashindano hayo yataendelea tena jumatano ambapo kutakuwa na shughuli pevu manchester united kucheza na barcelona mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani.

Nao ajax ya uholanzi itawaalika vibibi vizee vya turine italy timu ya juventus ambapo michezo hiyo pia itachezwa majira ya saa 4:00 za usiku.

YANGA SC IMEZINDUKA BAADA YA USHINDI WA MABAO 2-0 DHIDI YA AFRICAN LYON

Yanga sc imezinduka baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya african lyon jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Ushindi huo wa kwanza katika Ligi Kuu ndani ya mechi tatu, wakitoka kufungwa 1-0 na Lipuli na kutoa sare ya 1-1 na Ndanda FC, zote ugenini unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 71 baada ya kucheza mechi 30.

Maana yake, Yanga SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 11 zaidi ya Azam FC waliocheza mechi 30 pia wanaofuatia kwenye nafasi ya pili, mbele ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 57 za mechi 22 tu.

Mabao yote ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ebenezer Makambo ambaye yupo katika msimu wake wa kwanza tu tangu asajiliwe kutoka FC Saint Eloi Lupopo ya kwao.

Bao la kwanza alifunga dakika ya tano ya mchezo akimalizia pasi ndefu ya beki wa kati, Kelvin Patrick Yondan na la pili dakika ya 31 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Haruna Moshi ‘Boban’.
Kipindi cha pili Yanga SC iliendelea kupeleka mashambulizi langoni mwa African Lyon, lakini ikaishia kukosa mabao ya wazi mfululizo.

Powered by Live Score & Live Score App