Category Archives: Michezo na Burudani

TIMU YA KIKWAJUNI SPORT CLUB IMEPANIA KUIREJESHEA HADHI TIMU HIYO

Timu ya Kikwajuni Sport Club imepania kuirejeshea hadhi  Timu hiyo kama ilipokuwa ikitamba zamani. Hayo yamebainika leo hii baada ya kutembelewa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya kenya mahamoud abass.

Na kuweza kushiriki katika kutowa mafunzo kwa wachezaji wa timu hiyo.

Akizungunza na wandishi wa Habari za Michezo hapa visiwani katika mazoezi ya timu hiyo amesema Zanzibar inahistoria kubwa katika ukanda wa Afrika Mashiriki na kati katika mchezo wa soka hivyo vijana wa sasa wanapaswa kujifunza histori iliyowahi kuwekwa na wachezaji wa zamani .

Aidha Abassi  ambaye aliwahikuwa golikipa namba wani wa timu ya taifa ya kenya maarufu kama harambe stars amesema timu ya kikwajuni inahitaji kuwatunza wachezaji wake ili wapate kuisaidia timu ya Taifa ya Zanzibar pamoja na Taifa Stars.

Wachezaji pamoja na meneja wa timu hiyo wamesema ujaji wa mchezaji huyo imeweza kuinuwa ari ya wachezaji hapa nchini.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Mjini amesema kitu cha faraja kumuona mchezaji huyo wa zamani kukumbuka na kutowa mafunzo hapa visiwani.

TAMASHA LA PASAKA KWA MWAKA 2019 LINATARAJIWA KUFANYIKA JIJINI DAR-ES-SALAAM

 

Tamasha la pasaka kwa mwaka 2019 linatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21 april 2019 na kwa mwaka huu litaanzia jijini dares salaam, baadae na maeneo mengine ya nchi

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam, Mkurugenzi wa Msama promotion Alex Msama amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri, na kinachoendelea sasa ni mawasiliano na wasanii wataoshiriki wakiwamo wa kutoka nje ya nchi.

Aidha ndugu Msama ameelezea faida za tamasha hilo la pasaka kuwa mbali na kutoa burudani ni kuombea amani na umoja wa watanzania.

Katika kufuata maelekezo ya baraza la sanaa la taifa (basata) ndugu Msama ameelezea mwongozo uliotolewa juu ya wasanii wataoshiriki kwenye tamasha hilo huu kuwa ni wale wenye usajili wa basata hivyo amewasihi wasanii kufuata miongozo ya inayotolewa na chombo hicho.

BARAZA LA SANAA SENSA NA FILAMU KUSIMAMIA VYEMA KAZI ZA SANAA.

Naibu waziri wa vijana utamaduni sanaa na michezo Mhe. Lulu Msham Khamis ameliagiza baraza la sanaa sensa na filamu kusimamia vyema kazi za sanaa.

Akifungua mkutano wa   kujadili kazi za sanaa    katika ukumbi wa wizara hiyo Mhe Lulu amesema baraza hilo linawajibu mkubwa wa kusimamia kazi za sanaa  hivyo amelitaka  kuonyesha michezo inayoendana na maadili, silka pamoja na desturi za wazanzibari.

mwenyekiti wa baraza la sanaa sensa ya filamu na utamaduni bibi  Maryam Mohd Hamdani amesema  katika kuzingatia  haki za wasanii wamekuwa wakiandaa matamasha  pamoja na kutoa mafunzo  ili  kuendeleza jitihada  za wasanii hapa nchini.

Katibu wa chama cha wasanii waigizaji zanzibar salum stika    amesema  chama cha wasanii na waigizaji  katika kuhakikisha hilo linafanikiwa  mwaka huu kimejipanga   kutengeneza filamu  zenye kukubalika  na kuwa na ubora  ili ziweze kuingia katika ulimwengu wa ushindani.

  

(COSOZA) NA (NCAC) WAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SANAA PAMOJA NA KUBADILISHANA UZOEFU.

Afisi ya hakimiliki zanzibar (COSOZA) imesema mashirikiano waliyoanzisha baina yao na taasisi ya hakimiliki ya jamhuri ya watu wa china (NCAC) itasaidia kuimarisha ushiriakiano katika sanaa pamoja na kubadilishana uzoefu.

hayo yameelezwa na naibu katibu mkuu wizara ya vijana ,utamaduni ,sanaa na michezo Amour Hamili Bakari katika mkutano wa mashirikiano baina ya ofisi ya hakimiliki ya zanzibar na ofisi ya hakimiliki ya jamhuri ya watu wa china uliofanyika mazizini.

amesema pamoja na mashirikiano hayo pia ushirikiano huo utasaidia kutoa fursa kukabiliana na wizi wa kazi za sanaa

katibu mkuu wa  hakimiliki   zanzibar ( COSOZA) mtumwa ameir khatib amesema  taasisi ya hakimiliki ya china iko juu katika teknolojia  hivyo itasaidia zanzibar kuwa na mbinu madhubuti  za kupambana na uharamia wa kazi za wasanii hasa katika mitandao ya kijamii.

katibu wa chama cha wasanii na waigizaji zanzibar salum maulid amesema huu ni mwanzo mzuri kwa wasanii wa zanzibar kwani itasaidia kufungua milango na kukuza sana ya zanzibar kutokana na sanaa ya china kukua zaidi ukilinganisha na ya zanzibar

nae mkurugenzi mkuu wa taasisi ya hakimiliki ya china NCAC tang zhaozhi amesema ushirikiano huo ni muhimu baina ya nchi mbili hizi kwani utasaidia kulinda haki za wasanii ndani na nje ya Nchi.

 

Powered by Live Score & Live Score App