CCM NI CHAMA KINACHOSIMAMIA NA KUTEKELEZA KWA VITENDO MABADILIKO NDANI YA JAMII.

 

Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) tanzania bara mzee Philip Mangula amempokea aliekua mjumbe wa bodi ya wadhamini wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema muslim hassanali ambae amejiunga rasmi na ccm.

akizungumza katika mkutano wa kumpokea mwanachama huyo mpya jijini dar es salaam mzee mangula amesema ccm ni chama kinachosimamia na kutekeleza kwa vitendo mabadiliko ndani ya jamii.

amesema licha ya kukubali kukosolewa ccm inapanga na kutekeleza mikakati yake kwa kuangalia vipaumbele, hivyo kamwe haitokubali kutekeleza nje ya ilani ya ccm na nje ya yale waliyoahidi, kwani ndio yaliyowapatia kura na kuwafanya wakubadilike kwa wananchi.

akizungumza mara tuu baada ya kula kiapo cha uadilifu ndugu muslim hassanali amesema kila chama kina wajibu wa kujenga nchi, hivyo ameviasa vyama vya upinzani kutokuwa kikwazo katika kutekeleza wajibu huo.

mbali ya kuwa ni mjumbe wa bodi ya wadhamini ya chadema, muslim hassanali pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho na mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la ilala kwa tiketi ya chadema