CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA KIMETOA FURSA MPYA ZA KUIMARISHA UHUSIANO

 

Chama  cha  kikomunisti  cha  china  cpc  kimetoa  fursa  mpya  za kuimarisha  uhusiano wa  kimaendeleo   kati yake   na  nchi  za  afrika  ikiwemo  tanzania, ambao  utafungua  njia ya kufikia  maendeleo  yatakayodumisha  urafiki  kati ya china  na  bara  la  afrika .

Akitoa tathmini  ya mkutano mkuu wa  kumi  na tisa  wa  chama  cha  cpc   uliofanyika  mwezi  uliopita, balozi  mdogo  wa  china  aliyepo  zanzibar, xie xiaowu,  amesema katibu mkuu  wa chama   hicho  rais  xi  jinping   ameijenga   china   kuwa   na uhusiano wa kimataifa wa hali ya  juu  na kujijengea  heshima   na ukarimu  wa kuzisaidia  nchi  nyengine  kufikia hatua za kimaendeleo.

Amesema  mafanikiyo ya kiuchumi  yaliofikiwa na china  yameiwezesha kuimarisha  mikakati  ya kimaendeleo  kwa nchi za afrika ambapo  tanzania imefaidika na huduma za afya , ujenzi wa miundo  mbinu,huduma za kimaendeleo ya kijamii, kilimo ,utalii  na sekta  ya  elimu.

Balozi xie xiaowu  ameongeza  kuwa  uhusiano  uliopo  wa muda mrefu   kati  ya china  na  zanzibar  na tanziania  kwa ujumla  umekuwa na faida  kwani umechangia  kwa kiasi kikubwa kuimarika  kwa huduma za kijamii.