CHAMA CHA KIKOMUNISTI KUWEKA JINA LA RAIS XI JINPING NA FALSAFA YAKE YA KISIASA KATIKA KATIBA YA NCHI HIYO

Chama cha kikomunisti nchini china kimetangaza kwamba kitaliweka jina la rais xi jinping na falsafa yake ya kisiasa katika katiba ya nchi hiyo.
Tangazo hilo limetolewa leo wakati wa kufunga mkutano mkuu wa chama hicho ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano.
Mawazo ya xi kuhusu ”ujamaa na sifa ya china kwa ajili ya zama mpya”, yanatarajiwa kuwekwa pembeni mwa fikra za mao setung mwanzilishi wa china ya sasa ya kikomunisti na falsafa ya mrithi wake deng xiao ping.
Xi amesema atahakikisha anajenga jamii yenye ufanisi katika kuelekea china ya kisasa.
Hatua hii imeelezwa kuwa siyo ya kawaida na inasisitiza kasi na uthabiti ambao xi ameimarisha madaraka tangu alipochaguliwa mwaka 2012.
Kiasi ya wanachama elfu mbili na mia tatu wa chama hicho wanahudhuria mkutano huo mkuu mjini beijing, ambao hapo kesho watawachagua wajumbe wa kamati kuu ya chama.