CHAMA CHA MAKATIBU MAHSUSI TANZANIA (TAPSEA) KIMECHAGUA VIONGOZI WAPYA

 

Chama cha makatibu mahsusi Tanzania (TAPSEA) kimechagua viongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Mkutano mkuu wa sita uliombatana na uchaguzi mkuu umewachagua viongozi mbali mbali wakiwemo makamo mwenyekiti , katibu mkuu na pia kumrudisha tena madarakani mwenyekiti wa zamani Zuhura Songambele Maganga kuiongoza jumuiya hiyo  kwa kipindi chengine cha miaka mitatu.

Bi zuhura maganga amewashukuru wanachama hao kwa kumuamini na kumkabidhi tena madaraka hayo ili awezekuiendeleza mbele tapsea.

Mkutano mkuu wa tapsea ulianza tarehe  10 kwa kutanguliwa na kongamano ambapo tarehe 11 makamu wa Pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi aliufungua rasmi mkutano huo wa sita uliokuwa na kauli mbiu isemayo “ kuimarisha taaluma na uadilifu katika utendaji ,” inayohimiza makatibu mahsusi  kuzingatia uadilifu katika utendaji kazi ili kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.