CHAMA CHA MCHEZO WATU WENYE ULEMAVU KWENDA MICHEZO YA SPESHEL OLOMPINK

Jumla ya shiling milionkumi na tano zinahitajika kwa chama cha mchezo  watu wenye ulemavu wa akili kwa ajili ya kufanikisha safari ya kwenda kushiriki katika mashindano  michezo ya speshel olompink inayotarajiwa kufanyika nchini abudhabi.

Akizungumza mara baada  ya kumtambulisha na kuwaga   mwanafunzi  Salama Kheri wa kidato cha pili skuli ya mtende mwenye ulmavu wa akili ambae ataiwakilisha zanzibar kupitia mchezo wa riadha  huko kwa mkuu wa mkoa wa kusin tunguu.

Mwenyekiti wa bodi wa chama cha speshel olompik ambae pia ni Mkurugenzi wa idara ya watu wenye ulemavu zanzibar Bi Abeda rashid Abdalla amesema mwanafunzi huyo ambae ataondoka na ujumbe wa watu watatu wataungana  na wenzao watanzania bara  wanatajiwa kuondoka  tarehe 8/3/2019 mwezi ujao .

Amesema licha  ya    jitihada mbali mbali zinazochukuliwa na  chama cha watu wenye ulemavu wa akili na idara ya watu wenye ulemavu katika kufanikisha maandalizi ya safari hiyo lakini bado wanakabiliwa na  changamoto  kadhaa ikiwemo pesa za kujikimu ambapo ameiomba serekali na jamii inayoguswa na  watu wenye ulemavu kusidia  fedha hizo  ili waweze kufanikisha vyema safari hiyo

Nae katibu wa chama cha mchezo cha watu wenye ulemavu wa akili zanzibar Ndugu Tifay Mustafa Nahoda meitaka jamii kuondokana na dhana ya kwamba watuwenye ulemavu wa akili hawawezi kushiriki katika michezo amefahamisha watu wenye ulmavu ni sawa na jamii nyengine na wameweza  kuchukua midali za michezo kutoka nchi mbali bali .

Mkuu wa mkoa wa kusini unguja  Hassan Khatibu Hassn meipongeza idara ya watu wenye ulemavu  kwa jitihada zao wanazozifanya za kuibu vipaji vya watu wenye ulemavu na ameahidi kuendelea kushirikiana na idara hiyo katika kuwaletea maendeleo watu wenye ulmavu hasa katika sekta ya michezo.

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App