CHAMA CHA SKAUTI WANAWAKE TANZANIA KUYAFATA KWA VITENDO MAFUNZO WANAYOPEWA

Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mh. Samia suluhu hassan amewataka wanachama wa chama cha skauti wanawake tanzania kuyafata kwa vitendo mafunzo wanayopewa ili kuwajenga katika misingi bora.
Akizungumza katika hafla ya makbidhiano ya ulezi wa chama hicho huko katika ukumbi wa makumusho jijini dar es salam mama samia amesema wanawake wengi wenye mafanikio wamepitia katika vyama hivyo ambapo kwa sasa wamekuwa ni mfano wa kuigwa.
Aidha mh. Samia amesema kuwa lengo la chama hicho ni kutoa mafunzo na kumuendeleza mtoto wa kike katika kukabiliana na changamoto zinazomkabili ili kuweza kufikia malengo yake .
hata hivyo mh. Samia pia amempongeza aliyekuwa mlezi wa chama hicho mama salma rashid kikwete kwa kukilea chama hicho kwa umahiri mkuwa kwa muda wa miaka 12 na kutoa mchango wako kwa hali na mali ili kuona c hama hicho kinakuwa na mafanikio .
Nae aliyekuwa mlezi wa chama hicho mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne mama salma kikwete ambae pia ni mbunge wa kuteuliwa amesema ushirikiano na umoja waliokuwa nao ndio umemfanya kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kufikia malengo waliyojiwekea.
Mapema akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa bodi ya chama cha skauti wanawake tanzania bi anna abdalla amesema dira ya chama hicho ni kuwanuafaisha watoto wa kike ambao wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa kike kuweza kujiunga na chama hicho ili kuwandaa kuwa wazalendo na viongozi bora.
Chama cha skauti wanawake tanzania girl guide asssosiation kimeanzia nchini uingereza mwaka 1910 na tanzania kimeanza mwaka 1928 katika mkoa wa kilimanjaro kwa sasa chama hicho kina jumla ya wanachama zaidi ya laki moja katika mikoa mbali mbali nchini .