CHANAGAMOTO KUBWA ZA WATOTO WENYE ULEMAVU KATIKA MASUALA YA ELIMU

 

Wakati wadau wa asasi za kiraia wakikumbuka mauaji ya watoto wasio na hatia nchini afrika ya kusini mwaka 1976  wamesema bado kuna chanagamoto kubwa za watoto wenye ulemavu katika masuala ya elimu licha ya kuwepo kwa elimu mjumuisho.

Wakiadhimisha siku ya mtoto wa afrika iliokwenda sambamba na kauli mbiyu mpe elimu stahiki mtoto mwenye ulemavu ili asiachwe nyuma kimaendeleo  ,wadau hao wamesema miongoni mwa changamoto hizo ni upungufu wa walimu na  ukosefu wa wakalimani wa lugha za alama kwa watoto wenye ulemavu wa uziwi.

Wakitoa ushuhuda wao katika siku hiyo watoto hao wenye ulemavu wamesema wamekuwa wakipata shida kubwa kwa wenzao ambao hawana ulemavu na kuwaona kuwa si watu pamoja na kuwadharau.

Aidha wameitaka jamii kutowatenga watoto hao na kuona kuwa ulemavu si maajabu wala  mitihani ni kudra ya mwenyezimungu katika kuwatunuku viumbe wake.

Akitolea ufafanuzi baadhi ya maelezo ya wadau hao mwalimu juma  kutoka kitengo cha elimu mjumuisho katika wizara ya elimu na mafunzo ya amali  amesema kuhusu muda wa ufanyaji mitihani kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalum wamekuwa wakiongezewa muda wa nusu saa ili kuweza kukamilisha mitihani yao.

Siku ya mtoto wa farika huazimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16 mwezi wa sita ambapo chimbuko lake ni kuuawa kwa watoto mia sita wasio na hatia katika kijiji cha soweto  wakati wa utawala wa kibaguzi nchini afrika ya kusini.