CHANGAMOTO ZA USAFI KATIKA MAJUMBA YA WANANCHI MICHENZANI.

 

Mkurugenzi wa baraza la manispaa mjini nd. Aboud hassan serenge amelitaka shirika la nyumba zanzibar kushirikiana na baraza hilo katika kutafuta suluhu ya kuduu ya changamoto za usafi katika majumba ya wananchi michenzani.

Ameyasema hayo katika ziara ya pamoja kati ya watendaji wa manispaa ya mjini na watendaji wa shirika la nyumba ikiwa ni moja kati ya mikakati ya baraza hilo katika imarishaji wa usafi wa eneo hilo.

Serenge amesema kuwa hali ya usafi katika majumba ya michenzani hairidhishi hivyo mashirikiano baina ya taasisi hizo mbili yanahitajiki kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake ili kuimarisha hali ya usafi.

Amesema kuwa miundombinu ya utirirshaji wa maji machafu na maji ya mvua katika eneo hilo imekuwa chakavu hivyo inahitaji matengenezo ya haraka ili kurahisisha shughuli za usafishaji.

Aidha amewataka wafanya biashara na wananchi wanaofanya biashara na kulaza gari pembezoni mwa barabara kusimamisha vitendo hivyo huku akiamuru kufunga upitaji wa magari kwa njia zote zisiso rasmi kwani inachangia  kuharibu miundo mbinu ya usafi katika baadhi ya maeneo ya majumba ya michenzani.

Nae kamu mkurugenzi ufundi wa shirika nd. Ali juma ali ameahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa baraza la manispaa katika kutatua changamoto za usafi ndani ya maeneo hayo.

Aidha amelitaka baraza la manispaa kufanya makadirio ya gharama zinazohitajika katika uboreshaji wa miundombinu ya usafi ili kushikiana katika kufanya matengenezo