CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR ZBC

 

Waziri  wa habari utalii na mambo ya kale  mh mahmoud thabit kombo amesema  wizara   imekusudia kuzipa kipaumbele changamoto zinazoikabili shirika la utangazaji zanzibar zbc na kuziingiza  katika kipindi kijacho cha bajeti.

amesema    matayarisho ya bajeti hiyo tayari yamenzaanza ambapo  wizara imeshaziona changamoto za shirika  hilo   ambazo baadhi  zinahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka huku nyengine zikisubiri   bajeti  ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

mh  mahmoud ametoa maelezo hayo  wakati wizara yake ilipotembelea  vyombo vya  habari vya shirika la utangazaji zanzibar zbc  radio na tv  ikiwa na lengo la kujua utendaji wa shirika  hilo   pamoja na matatizo yanayolikabili shirika hilo ili yaweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Katika hatua nyengine waziri wa habari amewataka wafanyakazi wa shirika hilo kuendana na wakati wanapotoa taarifa za matukio  kwa wananchi hasa ukizingatia kwamba ni chombo cha serikali.

Mkurugenzi mkuu wa shirika  hilo  iman duwe amemueleza waziri wa habari kwamba kwa  kuwa shirika hilo limekuwa muhimili  mkubwa wa kuwapasha wananchi   kuwapatia  habari hivyo   changa moto  zinazolikabili shirika hilo ni ukosefu wa  kupatiwa mafunzo ya mara  kwa mara  kwa wafanyakazi wake licha ya vyombo hivyo kupiga hatua katika  mfumo wa urushaji  wa matangazo yake.