CHINA: HATUA YA MELI YA MAREKANI KUKARIBIA KISIWA NI UCHOKOZI MBAYA.

China: hatua ya meli ya Marekani kukaribia kisiwa ni uchokozi mbaya.

china imetaja hatua ya manowari ya marekani kupita karibu na kisiwa Triton kusini mwa Bahari ya nchi hiyo kuwa uchokozi wa kisiasa na Kijeshi.

Manowari ya Uss Stethem ilipita karibu na kisiwa hicho ambacho kinachozozaniwa pia na nchi za Vietnam na Taiwan.

Uchina ilijibu kwa kutuma Meli za Kijeshi na Ndege kuenda kisiwa hicho.

tukio hilo limetokea muda kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kufafanya mazungumzo ya simu.

China imekuwa kwenye mzozo wa umiliki wa maeneo ya Bahari na majirani zake kadha miaka ya hivi karibuni.