CHINA IMEUNGA MKONO VIKWAZO VIPYA VYA UMOJA WA MATAIFA DHIDI YA KOREA KASKAZINI

 

China imeunga mkono vikwazo vipya vya umoja wa mataifa dhidi ya korea kaskazini kufuatia majaribio yake ya makombora ya mwezi uliopita.

waziri wa mambo ya nchi za nje wa china wang yi amesema mzozo kati ya korea kaskazini na majirani zake   si wa kuridhisha.

Katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni marekani imeongeza msukumo kwa china ili kuunga mkono vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo lakini nchi hiyo imesisitiza jirani yake korea ya kaskazini kurudi katika mazungumzo kwa ajili ya kumaliza mzozo huo.