CHINA IMEZITOLEA WITO PANDE ZOTE ZIHESHIMU MAKUBALIANO KUHUSU MRADI WA NUKLIA WA IRAN

 

Jamhuri ya watu wa china imezitolea wito kwa mara nyengine tena pande zote husika kuwa ziheshimu makubaliano yaliyofikiwa kuhusu mradi wa nuklia wa iran.Wito huoumefuatia tangazo la marekani la kufungamanisha utekelezaji wa makubaliano hayo na vikwazo zaidi.Waziri wa mambo ya nchi za nje lu kang amesema makubaliano yaliofikiwa kwa shida ya mradi wa nuklea wa iran lazima yaheshimiwe. makubaliano hayo, amesema, yana umuhimu mkubwa katika kupatikana amani na utulivu katika mashariki ya kati.

Kabla ya hapo rais wa marekani donald trump amesema vikwazo vya kiuchumi dhidi ya tehran, vitasitishwa kwa muda wa siku 120 tu.Na amewatolea wito washirika wa nchi za magharibi wafikie makubaliano pamoja na marekani katika kipindi cha miezi minne kuhusu vikwazo zaidi katika makubaliano hayo.Pande zilizotia saini makubaliano hayo, umoja wa ulaya, urusi na china zimesema haziungi mkono wazo la kufanyiwa marekebisho makubaliano yaliyofikiwa.