CHINA KUENDELEA KUTOA NAFASI ZA MASOMO KWA WAZANZIBARI

Waziri wa habari utamaduni ,utalii,na michezo mhe, rashidi ali juma ameishauri jamhuri ya watu wa china kuendelea kutoa nafasi za masomo kwa wazanzibari hatua itakayosaidia kuwa na wataalamu wengi.
Akizungumza na ujumbe kutoka china ukiongozwa na naibu waziri wa habari wa china afisini kwake mhe, rashid amesema zanzibar bado inahitaji wataalamu wa fani mbali mbali na kwamba china ina uwezo wa kuwaandaa wataalamu hao.
Waziri wa habari amehimiza umuhimu wa kuimarishwa uhusiano kati ya jamhuri ya watu wa china na zanzibar kutokana na faida zake kwa mataifa mawili hayo.
Aidha naibu waziri wa china bw, gaowei amesema serikali inajivunia uhusiano wake na zanzibar na kueleza kwamba nchi yake itaialika zanzibar katika matamasha yake ya utamaduni kama ni sehemu ya kuifunza zanzibar namana ya kuenzi tamaduni zake.