CHINA WA KUISAIDIA TANZANIA NAFASI MAALUMU ZA MASOMO YA UDAKTARI

 

Waziri wa elimu sayansi na teknolojia mhe profesa joice ndalichako amesema mpango wa china wa kuisaidia tanzania nafasi maalumu za masomo ya udaktari utasaidia kuongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga madaktari wanafunzi wanaokwenda kozi nchini china, waziri ndalichako amesema changamoto ya upatikanaji wa matibabu inagusa maisha ya watanzania hivyo hatua hiyo itapunguza uhaba wa wataalamu wa afya.

Amemshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe dkt john pombe ,agufuli kwa kuguswa na changamoto ya uhitaji wa matibabu kwa idadi kubwa ya watanzania kufuatia  ujio wa meli ya madaktari kutoka china mwezi novemba mwaka 2017, na hivyo akaamua kupeleka maombi maalum  kwa rais wa china ili kuongeza nafasi maalumu kwa masomo suala litakalosaidia kuongeza wataalamu wa afya.

Naye balozi wa china nchini tanzania bi wang ke amesema nafasi hizo  ni mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu baina ya china na tanzania katika sekta ya afya ambapo toka mwaka 1964 serikali ya china ilianza kutuma timu ya madaktari kwa ajili ya kutoa huduma za afya tanzania bara na zanzibar ambapo takribani watu milioni 22 wameweza kufaidika na huduma hizo, huku  timu ya madaktari 32 wa kichina wanaendelea kufanya kazi katika hosptali ya taifa ya muhimbili  na katika hospitali ya mnazi mmoja zanzibar na pemba.

Jumla ya madaktari  50 wanakwenda kuhudhuria kozi za udaktari ambao kati ya hao 20 ni wa kozi ya muda mrefu  shahada ya juu na shahada ya uzamili yaani masters na phd na 30 ni wa kozi ya muda mfupi ambapo miongoni mwa mambo watakayojifunza ni pamoja na upandikizaji wa chembe za damu na ini, huduma za wagonjwa mahuututi, utoaji wa matibabu kwa njia ya mionzi, upasuaji wa kifua na moyo, ufundi mitambo ya hospitali, ugunduzi wa dawa za saratani,  ufamasia wa viwanda na mfumo wa viungo vya mwili na saratani ya damu kwa watoto