CHINA YAITAKA KOREA KASKAZINI KUSITISHA MAJARIBIO YA MAKOMBORA

 

 

China imeitaka korea kaskazini kusitisha majaribio ya makombora pamoja na teknolojia yake ya nyuklia ili kuondoa wasiwasi unaoendelea.

Ombi hilo limekuja baada korea kaskazini kufanya majaribio ya makombora manne siku ya jumatatu na kukiuka vikwazo vya kimataifa.

Waziri wa maswala ya kigeni wang yi amesema kuwa kwa makubaliano hayo marekani na korea kusini zitasitisha mazoezi ya kijeshi ya pamoja ambayo ni kikwazo kwa korea kaskazini.