CHINA YAPELEKA JESHI LAKE NCHINI DJIBOUTI

China imewapeleka wanajeshi wake watakaohudumu katika kambi yake ya kwanza ya kijeshi ya kigeni nchini djibouti.
Wizara ya ulinzi haikutoa maelezo kuhusu idadi ya vikosi vyake, lakini imesema wanajeshi wake wanatarajiwa kusaidia katika vita dhidi ya uharamia na operesheni za kulinda amani za umoja wa mataifa pamoja na za kiutu barani afrika na magharibi mwa asia.
Jeshi la china sasa linaungana na marekani, ufaransa, japan na nchi nyingine kadhaa zilizo na majeshi yake katika taifa hilo la kanda ya pembe wa afrika.