CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) KINAENDELEA NA KAMBI YA SIKU TANO MATIBABU YA MACHO

 

Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) kinaendelea  na kambi  ya siku tano  matibabu ya macho inayoendeshwa na wataalamu bingwa kutoka Pakistan na Saud Arabia huko Tunguu.

Akizungumzia kambi hiyo kaimu mkuu wa chuo hicho Mustapha Roshashi amesema lengo ni kuwasaidia wananchi wa zanzibar kupta tiba za maradhi mbalimbali kwa ukaribu.

Waziri wa  afya zanzibar Mhe Mahamoud Thabiti kombo  amefungua kambi hiyo na kueleza serikali inathamini juhudi za taasisi mbalimbali katika kusaidia utiajui wa huduma za afya kwa wananchi ikiwemo maradhi ya macho ambayo yanakuwa kwa kasi Zanzibar.

Takwimu za wizara hiyo zinaonesha kiasi ya wananchi elfu sita na mia tano wameathirika na upofu wa macho na wengine wapo hatarini kutokana na kukosa huduma ya matibabu mapema.