CYRIL RAMAPHOSA ANATARAJIWA KUAPISHWA NA KULIHUTUBIA TAIFA

 

Mwenyekiti wa chama tawala afrika kusini cha african national congress anc cyril ramaphosa anatarajiwa kuapishwa na kulihutubia taifa kwa mara ya kwanza kama rais wa afrika kusini hapo kesho baada ya kuteuliwa na bunge.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya rais jacob zuma wa nchi hiyo kuridhia shinikizo la chama chake cha anc na kung’atuka.

Kwa kufikia uamuzi huo rais huyo anayetuhumiwa kuhusika na rushwa, amekwepa kukabiliana na kura ya kutokuwa na imani naye iliyokuwa ipigwe bungeni hii leo.

Kabla ya hapo rais zuma alisema hatojiuzulu kwa sababu hajaambiwa makosa aliyoyafanya.

Uamuzi wa kujiuzulu rais zuma umepokolewa kwa furaha nchini afrika kusini kutokana na kumshutumu kiongozi kwa  kufanya ufisadi mkubwa ikiwemo kujenga nyumba yake binafsi kwa kutumia fedha za serikali.