DAWA ZA MALARIA ZINAZOPIGWA KATIKA NYUMBA HAZINA MADHARA

Serikali wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba imewatoa hofu wananchi kwamba dawa za malaria zinazopigwa katika nyumba zao hazina madhara  bali zinaangamiza mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya micheweni bi salama mbarouk khatib wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya tumbe ambao wamegoma kupigiwa dawa majumbani mwao

Amesema  lengo la serikali ni kuutokomeza ugonjwa wa malaria  na atasimamia ili kuhakikisha  zoezi hilo linafanikiwa na nyumba zote zinapigwa dawa.

Afisa kutoka kitengo cha malaria wizara ya afya pemba bakar omar khatib amesema wanachokifanya wanapofika kwenye nyumba ni kuwataka wakaazi wake kukunja vitu ambavyo vinaweza kuharibika na kuleta athari.

Mratibu wa mradi wa upigaji dawa faki haji faki  ametaka kuomngeza uhamasishaji ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Zoezi la upigaji wa dawa linafanyika katika shehia ambazo zimegunduliwa kesi za watu kuwa na virusi vya ugonjwa wa malaria.

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App