DEMOCRATIC YAMCHAGUA TOM PEREZ KUWA KIONGOZI MPYA

 

Wanachama wa democratic wamemchagua waziri wa zamani katika utawala wa obama tom perez kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho.

Kuchaguliwa kwa perez ambae ni mjumbe kutoka jimbo la minnesota kunafuatia raundi ya pili ya uchaguzi wa chama hicho uliofanyika jana.

Kiongozi huyo anatakabiliana na changamoto za kukiimarisha chama baada ya mgombea wake wa urais katika uchaguzi wa mwaka jana hillary clincton kushindwa uchaguzi huo.

Perez ameahidi kukibadilisha chama hicho na kuwafikia wanachama wa ngazi ya chini.