DIAMOND AMESEMA LENGO LA KUANZISHA KITUO CHA WASAFI TV NA RADIO NI KUWANYANYUA WASANII

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya tanzania abdul-nasib a.k.a diamond amesema lengo la kuanzisha kituo cha  wasafi  tv  na  radio ni kuwanyanyua wasanii waweze kupata nafasi ya kutangaza kazi zao.Diamond amesema mbali na kutoa ajira lakini pia chombo hicho kitaweza kuwanyanyua wasanii katika kupata nafasi ya kutangaza kazi zao wanazozifanya  pamoja na kuitangaza zanzibar na tanzania katika mataifa mbalimbali duniani kwani hatua hiyo itaweza kuipatia sifa nchin hasa katika sekta ya saana na utamaduni.ameiomba  serikali kutowa  msukumo  kwa  vijana ambao wanasifa  na vipaji vya kufanya kazi za usanii lakini wanashindwa kujiwezesha wenyewe na kuitaka serikali izidi kutoa mashirikiano kwa wasanii ili ndoto zao zisipotee bure.Waziri wa habari,utalii,utamaduni na michenzor rashid ali juma akizungumza katika halfa maalumu ya kumkabidhi hati ya usajili wa kituo kipya  cha wasafi tv na redio  amesema kuna umuhimu mkubwa wananchi kujitokeza katika  kufungua vituo vya habari nchini ili kuendeleza kwa  upatikanaji wa habari kwa wananchi zinazohusu maendeleo ya nchi yao.Hata hivyo mewataka wananchi wa zanzibar  na tanzania bara  kuendelea kuiunga mkono serikali ya mapinduzi zanzibar katika kuendeleza  kufungua vituo vya habari  kwani hatua hiyo itasaidia katika kuinyanyua tasnia ya habari hasa kwa kasi iliyopo hivi sasa ya utandawazi.Wakati  huo  huo  msanii  huyo  akiambatana  na  msanii  mwenzke  wa  amonaiz  amefanya  ziara  katika  studio  za  kurekodia  za  zbc  radio  na  kufika  katika  studio  ya  zbc tv  kuangalia  studio  mpya  na  ya  kisasa  na   kuishukuru  serikali  ya  mapinduzi  ya  zanzibar  kufanya  uwekezaji  mkubwa  wastudio  hiyo  hizo  za  kisasa na  kufanya  mahojiano  na  mwandishi  wetu.