DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI

 

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni kushika nafasi katika serikali.

Viongozi walioapishwa ni hassan khatib hassan kuwa mkuu wa mkoa wa kusini unguja, hemed suleiman abdalla kuwa mkuu wa mkoa wa kusini Pemba na Mwanajuma Majid Abdalla kuwa naibu katibu mkuu wizara ya kazi, uwezeshaji, wazee, vijana, wanawake na watoto (anaeshughulikia masuala ya wazee, vijana, wanawake na watoto).

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla hiyo ni makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali iddi, spika wa baraza la wawakilishi Zubeir Ali Maulid, mwanasheria mkuu wa zanzibar said hassan said, mawaziri na waziri wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar, katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi Dk. Abdulhamid yahya mzee.

Wengine ni mufti mkuu wa zanzibar Sheikh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, mkuu wa mkoa wa mjini amgharibi Ayoub Mohamed Mahmoud