DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMEZINDUA MFUMO WA UHAMIAJI MTANDAO (E-IMMIGRATION)

 

 

Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dk. John pombe magufuli amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi na utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia na wageni.

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika makao makuu ya idara ya uhamiaji kurasini jijini dar-es-salaam na kuhudhuriwa na rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mhe dkt ali mohamed shein, makamu wa rais mama samia suluhu hassan, waziri mkuu mhe kasim majaliwa, makamu wa pili wa rais zanzibar nhe balozi seif ali idi, wake za marais mama janet magufuli na mama mwana mwema shein, viongozi wa serikali, dini na vyama vya siasa na wananchi mbalimbali.

Akizungumza katika uzinduzi huo rais magufuli amesifu mafanikio yaliyofikiwa katika idara ya uhamiaji ukilinganisha na hali ilivyokuwa katika kipindi cha nyuma na akaahidi kuzishughulikia changamoto za taasisi hiyo.Aidha rais magufuli amehimiza watendaji wa idara hiyo kufanya kazi kwa weledi ikizingatiwa umuhimu wa taasisis hiyo katika mambo ya kiusalama, ulinzi na uchumi.Naye waziri wa mambo ya ndani  mhe mwigulu nchemba amesema uzinduzi huo utasaidia kuepusha mambo ya kugushi na kupunguza uhalifu wa kimataifa unaosababishwa na uwepo wa mifumo ya pasport isiyosomana.

Kamishina mkuu wa uhamiaji  dkt ana peter makakala amesema idara ya uhamiaji imedhamiria kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwa viongozi na wafanayakazi uzinduzi wa  pasrt hiyo ni mwanzo wa utekelezaji wa miradi mingine mikubwa ya idara hiyo.