DK. KHALID ATEMBELEA MAONESHO YA NANE NANE KIZIMBANI

 

 

Waziri wa fedha na mipango dk khalid salum mohamed amesema bidhaa zinazozalishwa na wakulima ni njia moja ya kupata masoko.

Akizungumza baada ya kutembelea maonesho ya nane nane kizimbani dr khalid amesema bidhaa nyingi zinaonesha kuridhishwana ubora kwani zinaonekana kuwa nzuri na za kuvutia na pia inaonekana wakulima wamepata elimu nzuri kwani zina ubora wa vifungashio.

Waziri huyo amesema kutokana na hilo serikali imekuwa ikiwahimiza wakulima kulima kilimo cha kisasa kwa vile tathmini na mikakati ya smz inayotolewa kwa wakulima ni nzuri hivyo amewahimiza wakulima kuja kizimbani kwenye maonesho wapate kujifunza zaid kwani kuna bidhaa na vitu tofauti.

Naibu waziri wa kilimo maliasili mifugo na uvuvi  dk makame ali ussi amewataka wakulima kutegemea mazuri na ushalishaji mzuri katika kutumia mbegu bora ili kupata mazao yenye rutba.

Akitoa maelezo kwa mh waziri wa fedha mkulima kutoka tasisi ya kilimo kizimbani khamis ali bakari amesema changamoto kubwa inayowakabili ni wadudu waharibifu wa mazao na kuiomba serikali kuliangalia vizuri tatizo hilo.

Nae mkulima wa mboga mboga  matunda amesema soko la pilipili lipo vizuri kwao.

Mh alitembelea mabanda mbali mbali na kupata maelezo juu ya maonesho  katika mabanda hayo.