DK SHEIN AKIZUNGUMZIA KUHUSU MAAZIMIO YA MKUTANO

Rais  wa  zanzibar  na  mwenyekiti wa  baraza  la  mapinduzi  ya  zanzibar  dk  ali  mohd  shein  amesema  mkutano wa  jumuiya  ya  nchi   zinazopakana   na  bahari  ya  hindi aliohudhuria  utaleta   mafanikio  makubwa  kwa   zanzibar   katika  sekta  tofauti hususan  masuala  ya   biashara  na  viwanda.

Akizungumza  na  waandishi  wa  habari  katika  uwanja  wa  ndege wa abeid  amani  karume  wakati  akitokea   nchini   indonesia  amesema  miongoni  mwa  mafanikio   kwa  wananchi  wa  zanzibar  ni pamoja   na  kusimamiwa  vyema   vipaumbele  walivyokubaliana  katika  ustawi  wa  wananchi  wa  zanzibar.

Hivyo  amesema  mkutano  huo ambao  umejikita  katika suala zima  la  amani  na  utulizo  kupashana  habari  kuhusiana  na majanga  makubwa  ,uvuvi   wa  bahari  kuu ,utalii na  kuzingatiwa  utamaduni  wa  nchi  husika  .

Dk  shein   akizungumzia   kuhusu  maazimio   ya   mkutano  huo  ni  kupambana  vikali   na  masuala  ya  ugaidi,  uharamia  na  watu  wanaovuka   viwango   kwa   nchi   21  wanachama  wa  jumuiya  hiyo.

Akizungumzia    maadhimisho  ya  siku  ya  wanawake   duniani  amewapongeza  akinamama  kwa  juhudi  kubwa  wanazozichukua  katika  kuhakikisha  wanashika  nyazifa  tofauti  ndani  ya  nchi katika  harakati  za  kujikomboa  kiuchumi.

. Mkutano  huo  ambao  ni  kwanza kufanyika kwa nchi  wanachama   umemchagua  mwenyekiti  wake  rais  wa  afrika  kusini   mh  jakop zuma  ili  kusimamia  maadhimio  walioafikiana kujua  namna  gani  wanafikia  malengo.