DK. SHEIN AMEWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KATIKA MAZISHI YA MWENYEKITI WA TUME YA UTUMISHI SERIKALINI

Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk. Ali mohamed shein amewaongoza viongozi na wananchi mbali mbali katika mazishi ya mwenyekiti wa tume ya utumishi serikalini marehemu othman bakari othman aliefariki dunia jana.
Marehemu bakari amezikwa katika makamburi ya mwanakwerekwe na ameshika nafasi mbalimbali katika chama na serikali ya mapinduzi ya zanzibar.
Miongoni mwa nafasi alizowahi kuzitumikia ni katibu msaidizi mkuu wizara ya habari upande wa televisheni, mkuu wa wilaya ya mjini na katibu msaidizi mkuu utafiti na tathmini ccm.
Marehemeu othman bakari ambae amezaliwa mwaka 1945 na kupata eleimu katika vyuo mbalimbali kikiwemo chuo cha diplomasia ameacha kizuka na watoto.